WENJE KUGOMBEA URAIS 2015

Ezekiel Wenje
MBUNGE wa Jimbo la Nyamagana jijini Mwanza, Ezekiel Wenje (Chadema) amesema atachukua fomu ya kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015. Wenje aliyasema hayo jana (juzi) alipohutubia maelfu ya wananchi wa mji wa Sengerema katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika uwanja wa Mnadani.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwashukuru wananchi wa wilaya hiyo hususan wakazi wa Kata ya Nyampulukano ya mjini Sengerema kwa kumchagua Diwani wa Kata hiyo Emanuel Mnwanizi(CHADEMA) katika uchaguzi mdogo wa udiwani mwezi uliopita.

Mbunge Wenje alikuwa ameongozana na wabunge watatu wa Chadema, akiwamo Dk. Antony Mbassa(Biharamlo Magharibi), Profesa Kulikoyela Kahigi (Bukombe) na Konchester Lwamlaza (Viti Maalumu).

Alisema atalazimika kufanya hivyo baada ya kuona nafasi hiyo imekuwa ya kuchezeachezea kwa huku utitiri wa watu wasio na sifa ya kugombea nafasi hiyo wakianza kujipenyezapenyeza.

“Makamanda niwapongeze sana…hakika nikisimama hapa sijui hata niseme nini kwa furaha niliyonayo kutokana na ushindi huu wa Nyampulukano,” alisema.

Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini

Akizungumzia tozo kadi ya simu Wenje alidai hali hiyo imesababishwa na umbumbumbu wa viongozi wanaotokana na Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kutotambua kiasi cha mapato yanayoingizwa na makampuni ya simu kila mwezi na ndiyo sababu ikaona mzigo huo wabebeshwe wananchi.

“Sekta ya mawasiliano nchini ndiyo sekta inayokuwa kwa kasi kwenye sekta za uchumi hapa Tanzania…kwa mwaka inakuwa kwa asilimia 24 lakini cha ajabu hakuna mapato ambayo serikali inayapata kupitia sekta hiyo,” alisema.



MTANZANIA

No comments

Powered by Blogger.