DAR KUSAHAU SHIDA YA MAJI



Mafundi wakiendelea kulaza mabomba yatakayotumika kusafirishia maji kutoka Mitambo ya Maji ya Ruvu Chini mpaka kwenye Tanki la kuhifadhia maji lililopo Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa mafundi hao wameshasambaza mabomba kwa umbali wa kilomita takribani 29 kati ya kilomita 55. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, mwaka huu. 
Timu ya mafundi ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu wakiwa kazini katika Ofisi ya Mitambo hiyo, mkoani Pwani.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 
Kaimu Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu, Mhandisi Deusdedit Rwegasira (Aliyevaa fulana la mistari) akiwaonesha Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango video ya namna miundombinu ya maji inavohujumiwa na baadhi wananchi wasiofuata taratibu zilizowekwa za kwa kujiunganishia maji kiholela.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu ilipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.
Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Kushoto) akiwaonesha Wataalamu wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mashine nne mpya zilifungwa na Serikali hivi karibuni walipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.
Viongozi wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Wapili Kushoto) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Watatu Kulia) wakionesha eneo la kusafishia maji katika Mtambo wa Ruvu Chini walipokuwa katika ukaguzi wa mtambo huo. Kushoto ni Mratibu wa ziara hiyo, Bibi Salome Kingdom.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua bomba lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa mitambo ya Ruvu Chini. Anayewaonesha ni Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Wapili Kulia).
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Watatu kushoto) kwenye lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa mitambo ya Ruvu Chini.Picha na Saidi Mkabakuli

No comments

Powered by Blogger.