MTU MMOJA ALIYEHUKUMIWA KIFO KWA KUNYONGWA AMEPONEA CHUPUCHUPU BAADA YA KUSAMEHEWA NA MAMAKE MWATHIRIWA NCHINI IRAN

Balal alimuua kwa kumdunga kisu Abdollah Hosseinzadeh miaka saba iliyopita.
 Mtu mmoja aliyehukumiwa kifo kwa kunyongwa nchini Iran baada ya kupatikana na hatia ya mauaji, ameponea chupuchupu baada ya kusamehewa na mamake mwathiriwa.
Mamake mwathiriwa alimzaba kofi mtuhumiwa na kisha kumasamehe dakika chache kabla ya kunyongwa
Mama huyo alimsamehe mtuhumiwa dakika chache tu kabla ya kuwekwa kamba shingoni.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Iran.
 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Picha za tukio hilo zilipigwa moja kwa moja na mpiga picha mmoja aliyenasa kila hatua ya tukio hilo ambalo liliwashangaza wengi nchini Iran na duniani kote.
Kisha alimuondoa kamba shingoni akisaidiwa na mumewe.
Shirika la habari la ISNA nchini Iran liliripoti kuwa mtuhumiwa huyo, kwa jina Bilal, alihukumiwa kifo baada ya kumuua kijana mmoja Abdollah Hosseinzadeh, wakati wawili hao walipokuwa wanapigana katika soko moja mjini Nour miaka saba iliyopita.
Bilal alifikishwa katika sehemu ya kunyongewa akiwa amefunikwa macho yake tayari kwa hukumu kutekelezwa siku ya Jumanne.
Lakini dakika ya mwisho kabla ya kunyongwa, mamake mwathiriwa Samereh Alinejad, alimwambia kuwa amemsamehe baada ya kuhutubia umati uliofika kushuhudia hukumu hiyo , kisha akamzaba kofi Bilal kabla ya Bilal kunusurika kifo.
Kabla ya mama huyu kumsamehe Balal alihisi hisia kali baada ya kukumbuka kifo cha mwanawe
 Samereh Alinejad, mamake marehemu Abdollah Hosseinzadeh, alimzaba kofi Balal dakika za mwisho alipokuwa anasubiri hukumu.

CHANZO: BBC SWAHILI

No comments

Powered by Blogger.