YALIYOJIRI KWENYE KITCHEN PARTY GALA MKOANI MWANZA

Mtaalam wa Maswala ya saikolojia,Aunt Sadaka akitoa somo kwa Wanawake wa jiji la Mwanza wakati wa hafla ya kina mama ya Familia Kitchen Party Gala.
Sehemu ya Kina mama wa Jiji la Mwanza wakifatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa kwenye Familia Kitchen Party Gala.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Mwasiti Almas akitoa burudani kwenye hafla hiyo.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wanawake wa Mwanza wamepata nafasi ya kuongea na Mama Victor,Aunt Sadaka na Getrude Mongela katika Familia Kitchen Party Gala. Shughuli imefanyika leo Jumamosi tarehe 19,katika ukumbi wa Gold Crest Hotel.
Ukiachana na maongezi kuhusu mahusiano na masuaka ya kina mama, vilevile wanawake walipata nafasi ya kupata huduma na ushauri wa Uzazi wa mpango, vipimo vya saratani/kansa ya mlango wa uzazi iliyotolewa bure na Familia kupitia PSI Tanzania.
 Kwa shilingi elfu kumi tu,kina mama walipata mafunzo,vipimo,chakula pamoja na burudani ya nguvu kutoka kwa Shaa na Mwasiti.





No comments

Powered by Blogger.