PICHA: MWANDISHI MWINGINE 'ACHINJWA' NA KIKUNDI CHA ISIS


 Mwandishi aliyechinjwa na ISIS Steven Sotloff.
Wapiganaji wa dola ya Kiislam ISIS wamesambaza picha za video katika mitandao kwa lengo la kuonyesha kuchinjwa kwa mwandishi wa habari raia wa Marekani Steven Sotloff ambaye ni mmoja wa mateka wanaoshikiliwa na wapiganaji hao. Mwandishi huyo Sotloff, mwenye umri wa miaka 31 ambaye alitekwa na wapiganaji hao mwezi August mwakajana.
Mwezi uliopita Sotloff alionekana mwishoni katika picha za video zilizoonyeshwa kuhusiana na kuchinjwa kwa mwandishi mwingine wa Marekani James Foley. Wapiganaji hao katika picha hizo pia wameonekana wakimtishia kumuua mateka mwingine anayedhaniwa kuwa ni raia wa Uingereza.
Mfuafi wa ISIS akishika kisu alichotumia kumchinjia Steven Sotloff.
Baada ya mauaji ya mwandishi wa awali Foley, mama mzazi wa mwandiashi wa Sotloff alitoa ombi maalumu kwa kiongozi wa wanajeshi hao Abu Bakr al-Baghdadi kutomuua mtoto wake. Msemaji wa Ikulu ya White House Josh Earnest amesema kuwa maofisa wa Marekani wanaendelea na uchunguzi wa ripoti hiyo.
Marekani hivi karibuni ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya ISIS nchini Iraq. Mwandishi wa masuala ya usalama wa BBC Frank Gardner amesema hatua hiyo ya wapiganaji wa ISIS ni kulipa kisasi kwa Marekani.

No comments

Powered by Blogger.