HAYA NDIO MAMBO YA KUFANYA ILI HUSIWARUHUSU WATU WENGINE WAFIKIRI BADALA YAKO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Huu ni ugonjwa unaotusumbua au kusumbua jamii yetu ya wasanii, wanamichezo na watu wa kawaida tu. Tunaishije au tunaishi kwa mawazo ya nani? Na ni nani anafikiri kwa niaba yetu? Kwenye makala hii inakupa faida ya wewe kujitambua na kuanza kufikiri mwenyewe kuhusu maisha yako, usiruhusu watu wengine au vyombo vya habari kumiliki utu wako na vile unavyotakiwa uwe.


1. Jenga utu wako wenye nguvu.Unatakiwa kujua wewe ni nani, unataka nini na kitu gani kitakufaa wewe. Usiruhusu watu wengine, au makampuni ya matangazo na vyombo vya habari kukuamulia namna unavyotakiwa kuonekana, kuhisi au mambo ya kufanya. Fanya kile ambacho kitakustahili wewe na maisha yako ili mradi tu huvunji sheria ya nchi na imani yako

2. Unatakiwa uwe na taarifa za kutosha. Tafuta habari za kutosha ili kujenga hoja za msingi. Hakikisha mawazo yako yanajengwa kwa kusoma, kuona na kusikiliza kwaajili yako mwenyewe. Chukua muda wa kutosha kufanya uchunguzi na kutafakari mambo yanayokuhusu.

3. Uwe tayari kubadilika. Tafuta suluhu ya mambo na kuangalia matokeo yake kwa kufuata mitizamo mbalimbali iliyo sahihi. Jaribu kujua faida na hasara na kutafuta uwezekano wa jambo kama upo na matokeo yake ni nini?

ENDELEA  KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


4. Angalia kama kuna namna ya kufuata mkumbo
Je wewe unashawishiwa na watu wanaokuzunguka au tamaduni fulani au watu fulani? Je wewe unaweza kufanya maamuzi sahihi na kwa uelewa wako? Je ni mara ngapi umefanya maamuzi ambayo si sahihi kwasababu ya kuwa sehemu ambayo si sahihi? Hebu jifanyie uchunguzi wako binafsi na uangalie maamuzi yako mengi yanatokana na nini? Nani ni mshawishi wako mkubwa na kwa nini?

5. Usifanye maamuzi kwa kuharakishwa, Woga, au Kujaribu kufuta makosa yako
Unatakiwa kuwa na ujasiri wa kusimamia unachokiamini na kilicho sahihi. Kama unataka kufanya kwasababu watu wengi wanafanya au kwaajili ya kuwafurahishwa watu fulani atakayeumia ni wewe na si wale ambao unajaribu kuwafurahisha.

Usiogope kushindwa au watu watakuonaje, fanya kitu sahihi na simamia hicho.

6. Faida ya kufikiri kuhusu maisha yako au wewe Mwenyewe
Inakujengea kujiamini, kufikia malengo na kuongeza uwezo wako wa kufikiri. Vile vile unajenga heshima yako binafsi kwa marafiki zako na watu wengine kile unachokiamini. Unakuwa unajua kitu gani ambacho vyombo vya habari vinataka uwe na wewe unajua namna ambavyo unatakiwa kufanya hivyo hauendeshi na vyombo vya habari.

No comments

Powered by Blogger.