SENTESI 3 ZA MAAJABU AMBAZO MWAJIRI ANATAKA KUSIKIA KWENYE INTERVIEW

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Sote tunaweza kukubaliana kuwa usaili ni njia isiyo kamilifu ya kumbaini mtu anayeomba kazi.
Kwa anayefanyiwa usaili, ni nguvu kujua iwapo anachokisema kinaendana na kile meneja mwajiri anakitafuta.


Lakini kuna sentesi chache zinazoweza kukupa alama nzuri. Ukipata nafasi hiyo wakati wa usaili, ni jambo zuri kujaribu kuzichomeka sentesi hizi sehemu.

1. “Nilifanikiwa sana kwenye hili siku za nyuma.”
Hii ni sentesi ambayo kwa hakika itabandika tabasamu kwenye sura ya anayekuhoji. Mameneja waajiri wanapenda kusikia kuwa si tu kwamba una ujuzi wanaoutafuta, bali uliuvuka. Zungumza pia mifano ya kipindi ulichofanikiwa kwenye jambo hilo. Hapo elezea mambo mazito uliowahi kuyafanya kwa mfano kusuluhisha mgogoro kwenye timu, kupata suluhisho ukiwa na data chache, kufanya kazi kwa kujitegemea na kukamilisha kazi kazi katika muda mfupi uliopewa.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


2. “Ninafurahia sana kuhusu nafasi hili.”
Kama ungekuwa unawafanyia usaili watu wawili wenye ujuzi unaofanana, kipi kinaweza kuwa kigezo cha uamuzi? Kwa waajiri wengi, uamuzi huja kutokana na jinsi muombaji huyo anavyofurahia nafasi na kampuni hiyo. Pamoja na kuwa na maana kubwa kuonesha kuwa unafurahia, unatakiwa kuwa na mambo ya kujazilizia kwa kufanya utafiti kuhusu kampuni hiyo.
Hakuna anayeweza kukuamini kama ukisema umefurahia mno kuhusu kazi hiyo au bidhaa hiyo lakini huwezi kuelezea kwanini ni bora kuliko ushindani.

3. “Tena nimezungumza na Peter kujifunza zaidi kuhusu hili.”
Bahati mbaya, huenda usiwe na kila kitu ambacho mwajiri anataka. Hakuna shida. Onesha jinsi ulivyo tayari kujifunza. Muhimu zaidi, unaweza kujifunza na kwamba tayari umeanza kujifunza.
Kufanya hili, kwanza tambua maeneo uliyo na udhaifu – labda unapungukiwa ujuzi mmoja ulioorodheswa kwene maelezo ya kazi.

Kisha, tafuta mtu au kitu ambacho kinaweza kukusaidia kuanza kujifunza na kujiimarisha kwenye eneo hilo. Kama swali hili likija wakati wa usaili, unaweza kusema umezungumza na au umeanza kujisomea.
Chanzo: Forbes

No comments

Powered by Blogger.