BREAKING NEW: RAIS KIKWETE APAGUA BARAZA LA MAWAZIRI MAJINA HAYA HAPA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungumza na vyombo vya habari leo jioni wakati anatangaza mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ametangaza mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri, ambalo ameliapisha jioni hii Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Akitangaza uteuzi huo muda mchache kabla ya Mawaziri hao kuapishwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema uteuzi huo unahusu pia kujaza nafasi mbili zilizoachwa wazi na Profesa Anna Tibaijuka na Profesa Sospeter Muhongo.

Profesa Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alieachishwa kazi kutokana na kuhusika kwake katika sakata la akaunti ya Tegeta Escrow.

Kwa upande wa Profesa Muhongo aliachia ngazi mwenyewe mapema leo,  kwa kile alichotaja kuipisha Serikali iendelee kuwatumikia Wananchi badala ya kuendelea na malumbano ya Escrow.


ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Katika mabadiliko hayo,sura mpya za manaibu mawaziri zimeingia na baadhi ya mawaziri wamehamishwa wizara.

Akitangaza Mabadiliko hayo, Balozi Sefue aliwataja mawaziri hao kama ifuatavyo.

MAWAZIRI

1. Mh. George Simbachawene - Waziri wa Nishati na Madini
2. Mh. Mary Nagu - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mahusiano na Uratibu)
3.Mh. Christopher Chiza - Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji
4. Mh. Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
5.Mh. William Lukuvi - Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi
6.Mh. Steven Wasira - Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
7.Mh. Samwel Sitta -Waziri wa Uchukuzi
8.Mh. Jenista Muhagama - Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge

MANAIBU WAZIRI
1. Stephen Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais - Muungano
2. Mh. Angela Kairuki -  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi
3. Mh. Ummy Mwalimu - Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
4. Mh. Anna Kilango - Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
5 . Mh. Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini

No comments

Powered by Blogger.