EWURA YATAKIWA KUFANYA UPYA UKOKOTOAJI NA KUPUNGUZA BEI YA MAFUTA ILI KUMNUSURU MWANANCHI WA KAWAIDA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji EWURA imetakiwa kufanya upya  ukokotoaji na kupunguza bei ya mafuta ili mwananchi wa kawaida anufaike na punguzo la bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia badala ya kuwanufaisha wafanyabiashara wakubwa wa  bidhaa hiyo pekee sambamba na kuangalia namna ya kuishirika sekta binafsi katika sekta ya gesi.
Agizo hilo la Bunge kupitia kwa kamati ya kudumu ya nishati na madini limetolewa bungeni mjini Dodoma na Mh .Juma Abdala Jjwayo wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo bungeni ili kuwapa fursa wananchi kunufaika na punguzo hilo badala ya kuwanufaisha wafanyabiashara wakubwa pekee  huku kamati ya kudumu ya bunge ya miundo mbinu Peter Serukamba akisisitiza ulaazima wa usafiri wa reli kufufuliwa.
 
Mara baada ya kuwasilishwa kwa taarifa hiyo baadhi ya wabunge waliopata fursa ya kuchangia wametaka serikali kutilia msisitizo kwenye miundo mbinu inayowagusa watanzania wote badala ya wale wenye kipato cha juu pekee,pia kupunguzwa kwa bei ya mafuta na nishati pamoja na kuhakikisha wafanyakazi wanaohudumia sekta ya reli wanalipwa stahiki zao kwa wakati.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 
Aidha pia wabunge wengi akiwemo mbunge wa simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka wamegusia suala la mradi wa usambazaji wa nishati ya umeme vijijini yaani REA na kutaka serikali kuhakikisha inatenga fedha za kutosha kuukamilisha mradi huo na kwamba suala la kupeleka na kusimika nguzo pekee halitoshi.

No comments

Powered by Blogger.