MKUU WA MKOA WA DODOMA AZUNGUMZIA HALI YA USALAMA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MIKUTANO YA CCM

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mh. Chiku Gallawa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), juu ya uwepo wa Mikutano Mikubwa ya Chama cha Mapinduzi katika Mkoa wake, inayotarajiwa kuanza rasmi kesho Julai 8, 2015, yenye agenda kuu ya kuchagua mgombea wa Urais atakatakayekiwakilisha chama cha CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu. Katika taarifa yake aliyoitoa leo Julai 7, 2015 Ofisini kwake, Mh. Gallawa amesema kuwa Mikutano hiyo itahusisha uwepo wa wageni wengi Mkoani Dodoma, hivyo kama Mkoa wamejipanga vyema kuwapokea wageni hao na kuwahudumia huku akiwatoa hofu kwa kuwahakikishia hali ya usalama kuwa ni ya uhakika. pia amewataka wale wote ambao hawahusiki na Mkutano huo na wala sio waalikwa, kutofika kabisa Mkoani Dodoma kwa sasa.
Sehemu ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mh. Chiku Gallawa wakati akizungumza nao juu ya uwepo wa Mikutano Mikubwa ya Chama cha Mapinduzi katika Mkoa wake.

No comments

Powered by Blogger.