HAYA NDIO MAZISHI YA MME WA KHADIJA KOPA ALIPOZIKWA BAGAMOYO HAPO JANA

Ndivyo anavyoonekana kusema Karima Chichi Mhandeni wa tatu kutoka kulia, akimfariji Khadija Kopa, katika msiba wa mume wake aliyezikwa jana Bagamoyo.
 Waombolezaji wakiwa katika msiba wa mume wa Khadija Kopa, jana mjini Bagamoyo.
Jeneza la Jafary Ally liliswaliwa mbele ya nyumba yake mjini Bagamoyo jana. Wa nne kutoka kulia ni mtoto wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Ridhiwan Kikwete, akiungana na waislamu wenzake kuuswalia mwili wa Diwani wa Kata ya Magomeni, mjini Bagamoyo.
 Safari ya kuelekea makaburini ilianza. Aliyebeba mwenye fulana ya mistari ni Yusuphed Mhandeni, Mchumi wa Kata ya Makumbusho CCM, jijini Dar es Salaam. Mazishi yake yalidhuhuriwa na watu wengi, wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Serikali pamoja na wasanii wengi waliokwenda kumpa pole Kopa.
 Khadija Kopa aliyefunikwa akifarijiwa kwa msiba wa mume wake mjini Bagamoyo.
 Mwili wa marehemu Jafary Ally ukiingizwa kaburini jana saa tisa alasiri mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

PICHA NI KWA HISANI YA HANDENI YETU

No comments

Powered by Blogger.