CHADEMA KIMESISITIZA MSIMAMO WAKE WA KUTOSHIRIKI MCHAKATO WA KUPIGA KURA YA MAONI YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA.

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kimesisitiza msimamo wake wa kutoshiriki kwenye mchakato wa kupiga kura ya maoni ya katiba mpya inayopendekezwa na badala yake kimewataka wanachama wake na watanzania kwa ujumla kuelekeza nguvu kwenye maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.
Kikisisitiza msimamo huo uliotolewa hivi karibuni na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (Ukawa) kimesema hakiko tayari kuona watanzania maskini wakipoteza rasilimali kwa jambo lililoharibiwa kwa manufaa ya watawala na chama kilichopo madarakani.
 
Mwenyekiti wa taifa wa chadema Mhe. Freeman Mbowe ameyasisitiza hayo wakati akiwahutubia maelfu ya wananchi wa kijiji cha Iselamagazi, jimbo la solwa wilayani Shinyanga ambapo pamoja na hayo amewashauri watanzania kuendelea kuubeza uongo uliokuwa ukisambazwa kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa Chadema ni chama cha wachaga na wakristo kwa kuwa ulikuwa na lengo la kuwagawa wananchi na walioko madarakani waendelee kuwatawala na kugawana rasilimali za nchi kwa faida yao binafsi. 
 
Naye naibu katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar Bw. Salum Mwalimu amewataka wananchi wa kanda ya ziwa kutowaunga mkono viongozi wa kisiasa mfano mzuri baadhia ya wabunge waliowachagua kwa ajili ya kuwatetea na kuwaletea maendeleo na badala yake kuwageuka na kuhamishia makazi yao Dar es Salaam na hivyo kukosa wa kuwawakilisha na kuwatatulia shida zao mbalimbali.
 
Awali wazee wa kimira wakabila la kisukuma wilayani Shinyanga wamemsimika Mhe. Feeman Mbowe kuwa mtemi wa kabila hilo kutokana na chama chake kuonekana kuwa mstari wa mbele kupigania haki, kupinga ufisadi na kutetea maslahi ya wananchi.

CHANZO: ITV TANZANIA

No comments

Powered by Blogger.