KUMBUKUMBU YA LEO: LEO TAREHE 22 SEPTEMBER NI SIKU YA KUZALIWA MWANAMAPINDUZI HAYATI ABDULRAHMAN MOHAMED BABU

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Marehemu Komredi Abdulrahman Mohamed Babu enzi za uhai wake

Komredi Professor Abdulrahaman Mohamed Babu alikuwa mwanasiasa,mwanamapinduzi msomi,mwandishi,mchumi, na ujamaa kwake ulikuwa ni mfumo wa maisha yake.
Tunapowataja na kukumbuka wakongwe wa siasa na wapambanaji waliosimama kidete kuhakikisha kuwa wafrika tuna jikomboa kutoka katika makucha ya ukoloni uwe mkongwe au ukoloni mambo leo,jina la marehem Abdulrahman Mohamed Babu (RIP)alitasahulika, ambaye kama angelikuwa hai leo tarehe 22 September ndio siku yake ya kuzaliwa.
Historia inatuelezea kuwa mwanamapinduzi marehem Prof. A.M.Babu alizaliwa 22 Sept 1924 huko kisiwani Unguja,Zanzibar, na alifariki dunia 05.08.1996, marehem Prof. A.M.Babu anakumbukwa kwa mengi pamoja na kuwa engineer wa mapinduzi ya visiwani 1964 yalimfanya sultani akimbie na kusahau kiremba kitandani

No comments

Powered by Blogger.